London,England.
LECEISTER CITY wametwaa ubingwa wa kwanza wa Ligi Kuu England baada ya wapinzani wao wa karibu Tottenham kulazimishwa sare ya mabao 2-2 katika mchezo mkali wa Ligi Kuu uliopigwa Jumatatu Usiku huko Stamford Blidge,London.
Licha ya Tottenham kuwa mbele kwa mabao 2-0 mpaka mapumziko kupitia kwa mabao ya Harry Kane na Son,Chelsea ililerejea kipindi cha pili kwa nguvu zote na kufanikiwa kusawazisha mabao yote mawili kupitia kwa Garry Cahil na Eden Hazard.
Kwa matokeo hayo Leceister City wamefanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kufikisha pointi 77 ambazo haziwezi kufikiwa na Tottenham yenye pointi 70 huku kukiwa kumebaki michezo miwili pekee ligi ifike mwisho.
0 comments:
Post a Comment