Addis Ababa,Ethiopia.
Ethiopia imetangaza kumtupia virago aliyekuwa kocha wake mkuu Yohannes Sahile kufuatia kuchoshwa na muendelezo wa matokeo mabaya ya timu yake ya taifa.
Taarifa kutoka chama cha soka cha nchi hiyo EFF (Ethiopian Football Federation) imesema Sahile ametimuliwa baada ya Ethiopia kufanya vibaya katika michezo inayoendelea ya kusaka tiketi ya kushiriki michuano ya AFCON 2017.
Ethiopia ambayo iko Kundi J pamoja na mataifa ya Lesotho,Ushelisheli na Algeria mapema mwezi Machi ilikutana na kichapo kizito cha mabao 7-1 toka kwa Algeria na kupoteza matumaini ya kufuzu michuano ya AFCON itayopigwa huko Gabon.
Wakati huohuo EFF imesema kuwa tayari imeshampata mrithi wa Sahile na itamtangaza baada ya siku chache zijazo pindi itakapokamilisha mambo machache yaliyobaki.
Sahile anakuwa kocha wa tatu kutimuliwa katika kipindi kisichozidi miaka mitatu.
0 comments:
Post a Comment