728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, May 02, 2016

    VPL:MECHI ZA YANGA V NDANDA,SIMBA V MWADUI ZABADILISHIWA TAREHE,SABABU ZA MSINGI ZATOLEWA

    Dar es salaam,Tanzania.

    Mechi ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Ndanda FC ya Mtwara na Young Africans umerudishwa nyuma kwa siku moja na sasa itachezwa Mei 14, 2016 badala ya Mei 15, 2016 kama ratiba ya awali inavyosomeka.

    Taarifa ya Bodi ya Ligi Kuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema sababu za kurudisha nyuma mchezo huo Na.218 utakaofanyika kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara ni kuipa timu ya Young Africans nafasi ya kujiandaa na kusafiri kwenda nchini Angola kwenye mchezo wa kimataifa wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika.

    Mbali ya mechi hiyo, kuna michezo miwili ambayo imesogezwa mbele kwa siku moja.Mechi hizo ni kati ya Simba na Mwadui ambayo sasa itachezwa Mei 8, 2016 badala ya Mei 7, 2016.

    Sababu za mchezo huo kusogezwa mbele ni kwamba Mei 7, 2016 kutakuwa na mchezo wa kimataifa utakaozikutanisha Young Africans dhidi ya Esperanca ya Angola kuwania Kombe la Shirikisho.

    Mchezo mwingine uliosogezwa mbele nikati ya Kagera Sugar dhidi ya Azam FC ambao sasa utafanyika Mei 8, 2016 badala ya Mei 7,2016.

    Sababu za mchezo huo kusogezwa mbele ni Uwanja wa Kambarage Shinyanga. Mei 7,2016 uwanja huo utakuwa na mchezo kati ya Stand United ya Shinyanga dhidi ya Coastal Union ya Tanga.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: VPL:MECHI ZA YANGA V NDANDA,SIMBA V MWADUI ZABADILISHIWA TAREHE,SABABU ZA MSINGI ZATOLEWA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top