Berlin, Ujerumani.
Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani Joachim Low leo jioni ametangaza kikosi cha awali cha wachezaji 27 kitakachoweka kambi kwa ajili ya kujinoa tayari kwa michuano ya Ulaya itakayopigwa nchini Ufaransa baadae mwezi Juni.
Katika kikosi hicho Low amemjumuisha kiungo wa Manchester United Bastian
Schweinsteiger,31 ambaye kwa kipindi kirefu amekuwa nje ya dimba akisumbuliwa na majeruhi.
Wengine waliojumuishwa katika kikosi hicho ni kiungo/mlinzi wa Liverpool Emre Can,Kiungo wa Arsenal Mesut Ozil,Mario Gotze.Kinda wa Bayern
Munich Joshua Kimmich na Julian Weigl wa Borussia Dortmund.
KIKOSI KAMILI NI:
Makipa: Manuel Neuer, Bernd Leno,Marc-Andre Ter Stegen.
Mabeki: Jerome Boateng, Emre Can,Jonas Hector, Benedikt Howedes, Mats Hummels, Shkodran Mustafi, Sebastian Rudy, Antonio Rudiger
Viungo: Karim Bellarabi, Julian Brandt,Julian Draxler, Sami Khedira, Joshua Kimmich, Toni Kroos, Mesut Ozil, Marco Reus, Leroy Sane, Andre Schurrle, Bastian Schweinsteiger, Julian Weigl
Washambuliaji: Mario Gomez, Mario Gotze,Thomas Muller, Lukas Podolski
0 comments:
Post a Comment