728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 20, 2016

    HIZI HAPA HABARI KUBWA 15 ZA USAJILI TOKA BARANI ULAYA IJUMAA YA LEO MEI 20,2016



    Lacazette:West Ham United imekwaa kisiki katika mbio zake za kumuwania mshambuliaji wa Lyon Mfaransa Alexandre Lacazette baada ya kuambiwa kuwa mkali huyo wa kupachika mabao hawezi kujiunga na klabu ambayo haichezi Ligi ya Mabingwa Ulaya.(Sky Sport)

    Van Gaal:Manchester United imeripotiwa kuwa inataka kumpa Ukurugenzi wa Michezo Mholanzi Louis Van Gaal na kisha kumpa Jose Mourinho kibarua cha kuinoa klabu hiyo iliyopoteza makali yake miaka ya hivi karibuni.(The Sun)

    Xhaka:Arsenal huenda hivi karibuni ikakamilisha usajili wa kiungo wa Borussia Monchengladbach Granit Xhaka baada ya rafiki wa karibu wa nyota huyo wa Uswisi ambaye pia ni mwandishi wa habari aitwaye Arthan Muhaxhiri kudai kuwa Xhaka ameelekea London kufanya mazumzo ya mwisho.(Daily Mirror)

    Morata:Juventus imeripotiwa kuanza kujiandaa na maisha bila ya mshambuliaji wake Alvaro Morata baada ya kudaiwa kuanza kuwafukuzia washambuliaji Edinson Cavani,Romelu Lukaku na Christian Benteke kuja kuwa wabadala wake.(Gazzetta dello Sport)

    Niguez:Barcelona imeachana na mpango wa kutaka kumsajili mshambuliaji kinda wa Atletico Madrid Saul Niguez,21 baada ya kuambiwa kuwa itawalazimu kutoa kitita cha €80m ili kumnasa nyota huyo wa Hispania.(Mundo Deportivo)

    Mori:Manchester United imeripotiwa kuanza kumfukuzia mlinzi wa kati wa Everton Ramiro Funes Mori lakini itakumbana na vita kali toka katika klabu ya Lazio ambayo nayo imeripotiwa kumfukuzia nyota huyo toka Argentina.(La Lazio Siamo Noi)

    Turan.Barcelona iko tayari kumwachia kiungo wake Arda Turan aondoke Camp Nou katika dirisha lijalo la usajili barani Ulaya.(Daily Mirror)

    Lukavu:Chelsea imeanza mazungumzo na Everton kwa ajili ya kuwasajili kwa mpigo nyota wawili wa klabu hiyo mshambuliaji Romelu Lukaku na mlinzi John Stones.(Het Laatste Nieuws)

    Lindelof: Manchester United imeripotiwa kutuma ofa ya £20m kwenda Benfica kwa ajili ya kumsajili mlinzi wa klabu hiyo Mswedeni Victor Lindelof,21.Vilabu vingine vilivyoripotiwa kumfukuzia mlinzi huyo anayefananishwa kiuchezaji na mlinzi wa zamani wa AC Milan Paolo Maldini ni Bayern Munich,Juventus, Paris Saint-Germain, Barcelona na Real Madrid.(Daily Star)

    Karius:Liverpool imekaribia kukamilisha usajili wa mlinda mlango wa Mainz 05 ya Ujerumani Loris Karius,22 kwa ada ya £4.7m.(The Guardian)

     Chilwell:Liverpool imeripotiwa kuwa karibu kumsajili mlinzi wa kushoto wa Leceister City Ben Chilwell,19 kwa ada ya £3m baada ya kuizidi ujanja Arsenal dakika za mwisho.(Daily Mirror)

    Mkhitaryan:Henrikh Mkhitaryan amezidisha uvumi kuwa anataka kujiunga na Arsenal baada ya kudaiwa kukataa mkataba mpya katika klabu yake ya Borussia Dortmund.(Bild)

    Vardy:West Ham United inataka kumsajili mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy baada ya kuchungulia mkataba wake na kukuta ana kipengele cha kuuzwa kwa £25m.(Goal.Com).

    Gollini:Everton imeonyesha nia ya kutaka kumsajili mlinda mlango wa Bologna Pierluigi Gollini,21 ili kuchukua nafasi ya mlinda mlango wake mkongwe Tim Howard anayetimkia Marekani.(Gazetta dello Sport)



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: HIZI HAPA HABARI KUBWA 15 ZA USAJILI TOKA BARANI ULAYA IJUMAA YA LEO MEI 20,2016 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top