728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 20, 2016

    AMUITA MBWA WAKE MESSI

    Messi na Isco uwanjani

    Madrid,Hispania.

    Hebu fikiria uko barabarani unatembea ghafla unaanza kusikia sauti ya mtu ikiita jina la mtu unayemfahamu.Unaamua kugeuka ghafla unakuta anayeitwa jina hilo ni mnyama tena Mbwa,Je utajisikiaje??


    Sasa sikia hii!!


    Isco akiogelea na Messi

    Kiungo wa Real Madrid Isco Alarcón amekiri kuwa amempa mbwa wake jina la staa wa FC Barcelona Muargentina Lionel Messi.

    Isco,24 akijibu swali aliloulizwa katika kipindi cha ‘El Hormiguero 3.0’ kupitia kituo cha Radio cha Antena 3 kwamba anazungumziaje uwepo wa uvumi kuwa Mbwa wake anaitwa Messi.

    Amedai wazo la kumuita Mbwa wake Messi limetoka zaidi kwa baba na kaka yake.Amesema "Kweli nina Mbwa anaitwa Messi.Sikumpa jina hilo kwa kupenda ila ilikuwa ni shinikizo tu kutoka kwa baba na kaka yangu.Wao ndiyo waanzilishi wa kila kitu.

    Isco ameongeza "Najisikia vibaya kuhusu jambo hilo lakini nitafanyaje, limeshatokea.Siongozani tena na Messi ninapokwenda matembezini.Namwacha nyumbani naogopa mtaani nitageuka kituko watu wakisikia namuita Mbwa jina hilo.Nanawa mikono yangu katika jambo hilo,natokea Real Madrid.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: AMUITA MBWA WAKE MESSI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top