728x90 AdSpace

  • Latest News

    Friday, May 06, 2016

    BAADA YA KUPATA POINTI 3 ZA AZAM FC,MBEYA CITY YATAKA NYINGINE TOKA TANGA

    Mbeya,Tanzania.

    Mwenyekiti wa Mbeya City fc, Mussa Mapunda amelipongeza shirikisho la soka Tanzania TFF kwa hatua yake ya kuipoka pointi 3 timu ya Azam Fc na kuziweka kwa timu yake kufutia makosa yaliyofanywa na timu hiyo ya Chamazi Complex kumchezesha mchezaji Erasto Nyoni aliyekuwa na zuio la kadi tatu za njano.

    Muda mfupi uliopita Mapunda ameimbia
    mbeyacityfc.com kwamba kwa kosa hilo City ilistahili kupata ushindi huo wa bao 3 na pointi 3 kama ambavyo kanuni za ligi zinavyoelekeza na kutoa angalizo kwa vilabu vyote vinavyoshiriki ligi kuu Tanzania bara kuongeza umakini katika kutunza kumbukumbu za adhabu au makosa mbalimbali kwa wachezaji wake.

    “Kwenye hili nalipongeza shirikisho, hakika wametenda haki, na ninawaomba waendelee kusimama kwenye misingi ya haki.Ni haki yetu kupata pointi 3 baada ya Azam fc kuchezesha mchezaji mwenye adhabu ya kadi 3 ambaye ni wazi hakustahili kucheza mchezo ule.Hata sisi tumekutana na hali hii katika nyakati tofauti lakini hatukuwahi kuthubutu kumchezesha mchezaji mwenye adhabu hata kama alikuwa ni muhimu kikosini” alisema.

    Akiendelea zaidi Mwenyekiti Mapunda
    alisisitiza vilabu kuwa makini na matukio ya aina hii huku pia akiikumbusha TFF kuendele kuchukua hatua kama hizi.

    Katika hatua nyingine Mapunda amesema kuwa bado anaamini TFF itaitendea haki City kwa kuchukua hatua kama hizi kwenye mchezo dhidi ya Coastal Union uliovunjika dakika mwisho za kipindi cha pili baada ya kutokea kwa vurugu kubwa uwanjani zilizosababishwa na mashabiki wa timu hiyo ya Tanga.

    “Naamini TFF watatutendea haki kwenye hili pia,mchezo ule ulikuwa na matukio mengi ya ajabu ambayo yalimfanya mwamuzi kushindwa kumaliza mchezo, risasi za moto zilipigwa uwanjani,sisi bado tunasubiri pointi tatu zingine kutoka kwenye mchezo ule, kwa sababu mnyonge mnyongeni haki yake mpeni”, alimaliza.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: BAADA YA KUPATA POINTI 3 ZA AZAM FC,MBEYA CITY YATAKA NYINGINE TOKA TANGA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top