728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, November 04, 2015

    WENGER:GUARDIOLA ALIKUJA NYUMBANI KWANGU KUOMBA NIMSAJILI


    London,England.

    Arsene Wenger amefichua kuwa alikaribia kumsajili Pep Guardiola mwaka 2001 kabla ya nyota huyo wa zamani wa FC Barcelona kutimkia Italia na kujiunga na Brescia.

    Akifanya mazungumzo kabla ya mchezo wa leo wa ligi ya mabingwa wa Ulaya dhidi ya Bayern Munich ambayo inafundishwa na Guardiola,Wenger amesema 

    "Pep alikuja nyumbani kwangu akitaka nimsajili na akitaka kuichezea Arsenal.Wakati huo alikuwa na miaka kati ya 30 au 31 kama sikosei.

    Haikuwezekana kumsajili kwani wakati huo Patrick Vieira na Emanuel Petit walikuwa na umri mdogo na walikuwa katika viwango bora sana kiuchezaji hivyo ilibadi niwalinde.

    Guardiola anaingia katika orodha ndefu ya nyota walikaribia kutua Arsenal lakini usajili wao ukakwama dakika za mwisho.Nyota wengine ni Lionel Messi,Cristiano Ronaldo na Zlatan Ibrahimovic.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WENGER:GUARDIOLA ALIKUJA NYUMBANI KWANGU KUOMBA NIMSAJILI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top