Las Vegas,Marekani.
Bondia wa Uingereza Amir Khan amekubali dili la kuzichapa na Manny Pacquiao April 9 mwakani huko Las Vegas,Marekani hii ni kwa mujibu wa baba wa mzazi wa bondia huyo aitwaye Shah Khan.
Kwa kipindi kirefu sasa Khan amekuwa akitafuata pambano la pesa nyingi baada ya pambano lake na Floyd Mayweather kuyeyuka miaka miwili iliyopita.Shah amedokeza kuwa baada ya kumkosa Mayweather wameamua kumgeukia Pacquiao ambaye muda siyo mrefu ataachana na mchezo huo na kujikita kwenye siasa.
Shah amesema nyaraka zote muhimu kusuhu pambano hilo tayari ziko mezani kwa promota wa Pacquiao,Bob Aram na mchezo huo utafanyika Marekani mwezi April mwakani.
0 comments:
Post a Comment