London,England.
Juan Cuadrado hataichezea tena Chelsea hii ni baada ya gazeti la Express la England kuripoti kuwa nyota huyo aliyeko kwa mkopo Juventus atauzwa jumla mwishoni mwa msimu huu.
Express limedokeza kuwa tayari vilabu vya Chelsea na Juventus vimefikia makubaliano ya kuuziana nyota huyo wa zamani wa Fiorentina kwa kitita cha £17.9m pindi mkataba wako wa mkopo utakapokuwa umefikia kikomo.
Cuadrado,27 alijikuta akitua kwa mkopo Juventus mwezi agosti baada ya kushindwa kuonyesha makali yake Stamford Blidge na kujikuta akikaa benchi katika michezo mingi ya Chelsea.
0 comments:
Post a Comment