728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, November 05, 2015

    VIDEO YA NGONO YAWAONDOA BENZEMA,VALBUENA KIKOSI CHA UFARANSA

    Paris,Ufaransa.

    Karim Benzema na Mathieu Valbuena wameachwa katika kikosi cha Ufaransa kilichotangazwa leo na kocha Didier Deschamps huku Hatem Ben Arfa akirejeshwa baada ya kutemwa mwaka 2012.

    Akikataa kujibu maswali yaliyo nje ya kikosi hicho Deschamps amesema ameamua kuwaacha nyota hao katika kikosi chake ili kuwapa nafasi ya kujiweka sawa kufuatia sakata la video ya ngono linalowakabiri.

    Akimuongelea Valbuena,Deschamps amesema ameamua kumuacha kiungo huyo ili aweze kuwa sawa kiakili licha ya jana jumatano kuichezea Lyon katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Zenit.

    Kwa upande wa Benzema ambaye jana alizuiliwa kwa masaa kadhaa na polisi wa jiji la Paris ili kutoa maelezo juu ya kuhusika kwake katika kesi hiyo yeye ameachwa kutokana na kuwa katika uchunguzi huku pia akizuiwa kuwa karibu na Valbuena ili kuepuka kuharibu upelelezi wa kesi hiyo ambayo imekuwa gumzo siku za hivi karibuni.

    Mbali ya kuwatema nyota hao pia Deschamps amewatema Dimitri Payet na Kurt Zouma huku Kingsley Coman wa Bayern Munich yeye akiitwa kwa mara ya kwanza kabisa katika kikosi hicho ambacho Novemba 13 kitakuwa Parc des France kuvaana na Ujerumani kisha siku nne baadae kitakuwa Wembley kukipiga na England.

    Kikosi kamili: Costil, Lloris, Mandanda,Digne, Evra, Jallet, Koscielny, Mangala,Sagna, Sakho, Varane, Cabaye,Diarra,Matuidi, Pogba, Schneiderlin, Sissoko, Ben
    Arfa, Coman, Gignac, Giroud, Griezmann na Martial

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: VIDEO YA NGONO YAWAONDOA BENZEMA,VALBUENA KIKOSI CHA UFARANSA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top