Tetesi na Paul Manjale.
Lanzini:Westham United inataka kumsajili moja kwa moja kiungo Muargentina Manuel Lanzini anayekipiga klabuni hapo kwa mkopo akitokea Al Jazira ya falme za kiarabu lakini dau lake la uhamisho la £8m linatarajiwa kukwamisha mpango huo baada ya Westham kulalamikia hali ngumu ya kifedha.
Anderson:Manchester United imeripotiwa kuwa iko tayari kutoa kitita cha £40m ili kuipika Bayern Munich katika mbio za kimnasa straika hatari wa AS Lazio Mbrazil Felipe Anderson,22.
Vardy:Leceister City imesema iko tayari kumuuza kinara wake wa mabao Jamie Vardy kwa kitita cha £15m kwenda klabu yoyote ile inayomuhitaji.Vardy,28 ndiye kinara wa mabao kwa sasa katika ligi kuu ya England akiwa na mabao 11 huku vilabu vya Tottenham, Liverpool, West Brom na Borussia Dortmund vikiripotiwa kuitaka saini yake.
Silva:Mlinzi wa Kibrazil Thiago Silva anaamaini kuwa anaweza kumshawishi nyota wa Real Madrid Cristiano Ronaldo akaachana na ndoto za kurudi tena Manchester United na badala yake akatua PSG.
Aguero:Straika wa Manchester City Muargentina Sergio Aguero ameripotiwa kuiweka roho juu klabu hiyo baada ya kudai kuwa anaweza kuachana na miamba hiyo ya England ikiwa itashindwa kupata mafanikio katika michuano ya klabu bingwa Ulaya.
Drogba:Kocha wa Chelsea Mreno Jose Mourinho amekataa mpango wa straika wake wa zamani Didier Drogba kutaka kurudi katika klabu hiyo kwa mkopo mwezi januari.Drogba,37 kwa sasa anaichezea Montreal Impact ya Marekani akiwa amefunga magoli 11 katika michezo 11.Habari zinasema Drogba huenda akajiunga na Bologna ya Italia baada ya Mourinho kumtosa kutokana na wakati huo ligi ya Marekani kuwa mapumzikoni.
0 comments:
Post a Comment