728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, November 01, 2015

    LIGI YA MABINGWA AFRIKA:TP MAZEMBE YAUKARIBIA UBINGWA YAITUNGUA USMA 2-1,SAMATTA ATUPIA 1 AWA MFUNGAJI BORA WA MICHUANO.



    Algers, Algeria.

    TP Mazembe iko karibu kabisa kuutwaa ubingwa wa michuano ya vilabu bingwa Afrika baada ya jana jumamosi kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya USMA katika mchezo wa kwanza wa fainali uliopigwa huko Algeria.

    TP Mazembe ambao ni mabingwa mara nne wa michuano hiyo walipata goli la kuongoza dakika ya 27 kupitia kwa Rainford Kalaba aliyefunga akiunganisha krosi safi ya Thomas Ulimwengu.Baadae Kalaba alilimwa kadi nyekundu baada ya kumpiga usoni mchezaji mmoja wa USMA na kuifanya TP Mazembe kumaliza kipindi cha kwanza ikiwa pungufu.

    Goli la pili la TP Mazembe limefungwa na Mtanzania Mbwana Samatta dakika ya 77 kwa mkwaju wa penati uliotolewa baada Mbwana Samatta kuangushwa katika eneo la hatari na nahodha wa USMA Nacereddine Khoualed.Kabla ya hapo Samatta alikosa penati baada ya kuzidiwa ujanja na kipa wa USMA Mohamed Zemmamouche.Kufuatia goli hilo Samatta amefikisha magoli 7 na moja kwa moja anakuwa mfungaji bora wa michuano hiyo.

    Goli la kufutia machozi la USMA limefungwa dakika ya 88 na Mohamed Seguer aliyekuwa ameingia muda mfupi akitokea benchi.

    Mchezo wa fainali ya pili unatarajiwa kuchezwa Novemba 8 huko Lubumbashi,Congo nyumbani kwa TP Mazembe na mshindi atapata dola milioni 1.5 pamoja na kuiwakilisha Afrika katika michuano ya vilabu bingwa duniani huko Japan baadae mwaka huu.

     VIKOSI

    USM Alger: Zemmamouche, Benayada, Boudebouda, Mazari, Khoualed, El Orfi, Ferhat, Koudri, Nadji, Beldjilali, Benmoussa

    TP Mazembe: Kidiaba, Frimpong, Kimwaki, Coulibaly, Boateng, Diarra, Sinkala, Kalaba, Ulimwengu, Samatta, Traore
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: LIGI YA MABINGWA AFRIKA:TP MAZEMBE YAUKARIBIA UBINGWA YAITUNGUA USMA 2-1,SAMATTA ATUPIA 1 AWA MFUNGAJI BORA WA MICHUANO. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top