Torino,Italia.
Juventus imepanda mpaka nafasi ya 10 katika msimamo wa ligi ya Seria A baada ya jana jumamosi kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Torino katika mchezo mkali wa mahasimu wa jiji la Turin maarufu kama "Derby Della Molle" uliopigwa katika dimba Estadio Juventus.
Mabao ya Juventus yamefungwa na Paulo Pogba dakika ya 19 huku lile la ushindi likifungwa na Juan Cuadrado dakika ya 93 ya mchezo akiunganisha krosi safi ya Alex Sandro.Bao la Torino limefungwa na mlinzi Cecare Bovo dakika ya 51.
Katika mchezo mwingine uliopigwa huko Giuseppe Meazza, Inter Milan imefanikiwa kukalia kiti cha uongozi wa Seria A ikiwa na pointi 24 kibindoni baada ya kuitungua AS Roma kwa bao 1-0 shukrani za dhati zimuendee kiungo Gary Medel aliyefunga dakika ya 31 kwa shuti kali akimalizia kazi nzuri ya mshambuliaji wa zamani wa Manchester City Stephan Jovetic na kuishusha AS Roma mpaka nafasi ya pili ikiwa na ponti 23 baada ya kushuka dimbani mara 11.
0 comments:
Post a Comment