728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, November 02, 2015

    STARS KUPAA ASUBUHI HII KUELEKEA SAUZI KUWEKA KAMBI TAYARI KUIVAA ALGERIA


    Timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inaondoka leo jumatatu Saa 4:00 asubuhi kwenda Johannersburg, Afrika Kusini kuweka kambi ya siku 10 kujiandaa na mtanange dhidi ya Algeria katikati ya mwezi ujao.

    Kikosi kinachotarajiwa kupaa leo ni 

    Makipa:
    Aishi Manula (Azam FC), Ally Mustafa ‘Barthez’ (Yanga SC) na Said Mohammed (Mtibwa Sugar). 
     
    Walinzi:Shomary Kapombe (Azam FC), Juma Abdul, Mwinyi Hajji Mngwali, Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kelvin Yondan (Yanga SC), Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Hassan Isihaka (Simba SC) na Salim Mbonde (Mtibwa Sugar). 
     
    Viungo:Himid Mao, Mudathir Yahya, Salum Abubakar ‘Sure Boy’, Frank Domayo (Azam FC), Jonas Mkude, Said Ndemla (Simba SC) na Salum Telela (Yanga SC). 

    Washambuliaji ni Farid Mussa, John Bocco (Azam FC), Simon Msuva, Malimi Busungu (Yanga SC) na Ibrahim Hajib (Simba SC). 
     
    Washambuliaji Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DRC watajiunga na kambi baada ya mchezo wa marudiano Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya USM Alger wikiendi hii mjini Lubumbashi, wakati Mrisho Ngassa wa Free State Stars ya Afrika Kusini atajiunga na kambi mjini Johannersburg.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: STARS KUPAA ASUBUHI HII KUELEKEA SAUZI KUWEKA KAMBI TAYARI KUIVAA ALGERIA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top