Barcelona,Hispania.
Nyota wa FC Barcelona wamejikuta wakiingia lawamani baada ya kufanya vitendo vya ajabu katika viungo vya makao makuu ya klabu ya Getafe mara baada ya mchezo wa jumamosi iliyopita ambao FC Barcelona iliibuka na ushindi wa mabao 2-0.
Wachezaji wa FC Barcelona wakiongozwa na Neymar,Pique na Suarez walianza vituko baada ya kuvamia katika chumba cha mahojiano wakiwa wamevaa vinyago na mavazi ya ajabu na kumfanya nyota wa Getafe Victor Rodriquez ashindwe kuendelea na mahojiano aliyokuwa akifanya na AS.
Tukio jingine walilolifanya nyota wa FC Barcelona na kunaswa na Soka Extra ni uchafuzi wa mkubwa katika vyoo ambapo licha ya kuacha mazingira yakiwa siyo rafiki bali pia walimwanga mwaga rangi nyekundu ambayo kwa mbali ilionekana kama damu na kuwafanya maafisa wa Getafe kuita waandishi wa habari wajionee hali ile.
0 comments:
Post a Comment