London,England.
Fabregas akiwa na Mourinho wakisherekea ubingwa wa ligi kuu msimu uliopita
HAPANA!! hii ndiyo kauli ya kiungo Cesc Fabregas baada ya kushutumiwa kuongoza mgomo ndani ya klabu ya Chelsea.
Cesc Fabregas ametumia ukurasa wake wa Twitter kukanusha habari zilizoenea kuwa anaongoza mgomo wa chini chini ndani ya klabu hiyo na kupelekea matokeo mabaya ili kukakikisha kocha Jose Mourinho anatimuliwa kazi.
Fabregas ambaye siku za hivi karibuni amekuwa akituhumiwa kuwa anacheza chini ya kiwango amesisitiza kuwa habari hizo ni za kizushi na zinataka kumgombanisha na kocha Jose Mourinho.
Fabregas ameenda mbali zaidi na kuongeza kuwa bado ana furaha ya kuendelea kucheza chini ya kocha Mourinho na ikiwa kocha huyo atafukuzwa kazi klabuni hapo basi asichukuliwe kama msababishi.
0 comments:
Post a Comment