Dar es salaam,Tanzania.
Vilabu vya Simba na Yanga vimewapa mapumziko ya siku kadhaa nyota wao katika kipindi hiki ambacho ligi kuu ya Vodacom ikiwa imesimama kwa muda kupisha maandalizi ya timu ya taifa (Taifa Stars) ambayo Novemba 14 ya mwezi huu itavaana na Algeria katika mtanange wa kusaka tiketi ya kuingia katika hatua ya makundi ya kusaka nafasi ya kushiriki michuano ya kombe la dunia 2018 nchini Urusi.
Simba imetoa likizo ya siku 17 huku Yanga kupitia kwa afisa habari wake Jerry Muro ikiripotiwa kutoa likizo ya siku 10 na kuwata kuripoti kambini Novemba 12 kuanza maandalizi ya michezo ikiyobaki ya mzunguko wa kwanza.
0 comments:
Post a Comment