Manchester, England
Manchester United imeripotiwa kuwa haina haraka ya kumpa mkataba mpya Marouane Fellaini licha ya kiungo huyo kuonyesha nia ya kutaka kuendelea kubaki Old Trafford kwa kipindi kirefu zaidi.
Habari za ndani zinasema kuwa maafisa wa Manchester United wamekuwa wazito kumpa mkataba mpya Fellaini,27 kutokana na ukweli kwamba nyota ameshindwa kung'ara klabuni hapo huku akiwa amecheza michezo 32 pekee tangu ajiunge na klabu hiyo miaka miwili na nusu iliyopita akitokea Everton kwa ada ya £28m.
Kufuatia sintofahamu hiyo vyombo vya habari vya England vimeripoti kuwa Manchester United inapanga kumpiga bei kiungo huyo mkali wa mipira ya vichwa mara baada ya michuano ya Euro 2016.
Manchester United inataraji kuitumia michuano ya Euro kama sehemu ya kumuuza Fellaini ambaye amebakisha miezi 30 katika mkataba wake wa sasa.
0 comments:
Post a Comment