Lubumbashi,Congo.
LEO ni leo huko Lumbumbashi Congo mida ya saa 9:30 (Tanzania 10:30 Mchana) ambapo miamba ya soka ya nchi hiyo TP Mazembe itashuka katika dimba lake la nyumbani kuivaa USM Alger ya Algeria katika mchezo wa pili wa fainali ya vilabu bingwa Afrika.
TP Mazembe inaingia uwanjani ikiwa na faida ya ushindi wa mabao 2-1iliyoupata katika mchezo wa kwanza ulipigwa wikendi iliyopita huko Algeria kupitia kwa mabao ya Mzambia Rainford Kalaba na Mtanzania Mbwana Samatta ambaye huenda akaibuka mfungaji bora wa michuano hiyo baada ya kuwa amefunga mabao saba.
Mchezo huo utakaorushwa LIVE na kituo cha Supersport (9) unatarajiwa kuwa ni wa vuta ni kuvute kutokana na aina ya soka la kasi linalotandanzwa na vilabu hivyo ambavyo vitawakosa baadhi ya nyota wao muhimu.Mazembe itawakosa Jean Kasusula aliye majeruhi na Rainford Kalaba anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu USMA wao watakuwa bila ya Youcef Belaili aliyefungiwa baada ya kugundulika anatumia madawa ya kuongeza nguvu na Hocine El Orfi anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu.
Ikiwa TP Mazembe watafanikiwa kushinda au kutoka sare mchezo wa leo watatawazwa kuwa mabingwa wa Afrika kwa mara ya tano huku Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wakiweka historia ya kuwa Watanzania wa kwanza kutwaa taji hilo tangu lilipoanzishwa mwaka 1965.
0 comments:
Post a Comment