Manchester,England.
Manchester United imemaliza ukame wa kucheza dakika 404 bila kufunga bao baada ya jana usiku kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya CSKA Moscow katika mchezo mkali wa ligi ya mabingwa uliopigwa katika dimba la Old Trafford,Manchester.
Bao la pekee la ushindi la Manchester United limefungwa kwa kichwa dakika ya 79 na nahodha Wayne Rooney kufuatia pasi maridadi ya kinda Jesse Lingard.
Bao hilo limemfanya Rooney afikisha mabao 237 na kuwa sawa na gwiji wa zamani wa klabuni hiyo Denis Law huku akihitaji mabao 12 zaidi ili kuifikia rekodi ya Bobby Charlton ya mabao 249 na kuwa mfungaji wa muda wote.
Kwingineko vilabu vya Manchester City na Real Madrid vimekuwa vilabu vya kwanza kutinga hatua ya 16 bora baada ya kuibuka na ushindi katika michezo yao ya hapo jana.
Manchester City iliilaza Sevilla kwa mabao 3-1 huku Real Madrid ikiizidi ujanja PSG na kuzaba bao 1-0 shukrani kwa goli la mlinzi Nacho.
Matokeo mengine
Real Madrid 1 – 0 PSG
Man Utd 1 – 0 CSKA
FC Astana 0 – 0 Atl Madrid
Sevilla 1 – 3 Man City
Shaktar Donsk 4 – 0 Malmö FF
PSV Eindhoven 2 – 0 VfL Wolfsburg
Benfica 2 – 1 Galatasaray
B M’gladbach 1 – 1 Juventus
0 comments:
Post a Comment