London,England.
Arsenal imesafiri kwenda kuivaa Bayern Munich bila ya mlinzi wake mahiri wa kulia Hector Bellerin.
Bellerin,20 ameshindwa kusafiri na kikosi hicho kilichoondoka leo jioni baada ya kupata jeraha la groin wakati akifanya mazoezi ya mwisho kabla ya kupaa kwenda Munich,Ujerumani kuivaa Bayern katika mchezo wa pili wa kundi F.
Kocha Arsene Wenger anatarajia kumtumia mlinzi mkongwe Mathieu Debuchy kuziba pengo hilo huku pia akiwa amemjumuisha kikosini kinda mwenye miaka 17 Jeff Reine-Adelaide ili kuongeza nguvu upande wa kulia kutokana na klabu hiyo kuwa na majeruhi wengi wa upande huo.
Arsenal inaingia kuivaa Bayern Munich ikiwa bila ya nyota wake tisa ambao wanakabiliwa na majeruhi mbalimbali.Nyota hao ni Hector Bellerin,Aaron Ramsey,Alex Oxlade Chamberlain,Theo Walcott,David Ospina, Jack Wilshere, Danny Welbeck, Tomas Rosicky na nahodha Mikel Arteta.
0 comments:
Post a Comment