London,England.
Mlinzi wa kushoto wa Arsenal Kieran Gibbs ameingia katika vitabu vya kumbukumbu vya ligi kuu ya England (EPL) baada ya goli lake dakika ya 77 dhidi ya Tottenham kuwa ni goli la 24,000 tangu kuanza kwa ligi hiyo mwaka 1992.
Gibbs aliyeingia uwanjani kuchukua nafasi na Joel Campbell alifunga goli hilo baada ya kuuwahi mpira mrefu uliopigwa na Mesut Ozil na kuisaidia Arsenal kupata sare ya goli 1-1.
Goli la kwanza la ligi kuu ya England lilifungwa na mshambuliaji Brian Deane na kuisaidia Sheffield United kuibuka na ushindi wa magoli 2-1 dhidi ya Manchester United katika dimba la Bramall Lane.
Nyota wengine ambao wameingia katika vitabu vya ligi kuu England ni
1 – Brian Dean (Sheffield United)
100 – Eric Cantona (Leeds)
1,000 – Mike Newell (Blackburn)
5,000 – Chris Sutton (Blackburn)
10,000 – Les Ferdinand (Tottenham)
15,000 - Moritz Volz (Fulham)
20,000 - Marc Albrighton (Aston Villa)
24,000 - Kieran Gibbs (Arsenal)
0 comments:
Post a Comment