Sevilla,Hispania.
Real Madrid imekumbana na kipigo cha kwanza La Liga baada ya hapo jana usiku kulala kwa mabao 3-2 toka kwa Sevilla katika mchezo mkali uliopigwa Sanchez Pizjuan.
Magoli ya Sevilla yamefungwa na Ciro Immobile,Ever Banega na Fernando Llorente huku Sergio Ramos na James Rodriguez wakiifungia Real Madrid.
Kufuatia kipigo hicho Real Madrid imeenguliwa kileleni na FC Barcelona ambayo katika mchezo wa mapema ikiwa katika dimba lake la Camp Nou iliibuka na ushindi wa magoli 3-0 dhidi ya Villarreal.
Magoli ya FC Barcelona yamefungwa na Neymar aliyefunga mara mbili huku Louis Suarez akifunga kwa mkwaju wa penati baada ya Munir El Haddadi kuangushwa na Jaume Costa.
Katika mchezo mwingine Atletico Madrid imeibuka na ushindi finyu wa goli 1-0 dhidi ya Sporting Gijon shukrani kwa goli la dakika za mwisho la Antoine Griezmann.
0 comments:
Post a Comment