728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, April 09, 2017

    Pepe aipa pigo Real Madrid


    Paul Manjale.

    MLINZI wa kimataifa wa Ureno,Képler Laveran Lima Ferreira maarufu kama Pepe ameipa pigo klabu yake ya Real Madrid baada ya kuripotiwa kuwa atakuwa nje ya uwanja kwa majuma kadhaa kutokana na kuvunjika mbavu mbili za upande wake wa kushoto kwenye mchezo wa jana Jumamosi wa ligi La Liga dhidi ya Atletico Madrid ulioisha kwa sare ya bao 1-1 dimbani Santiago Bernabeu.

    Pepe,34,mfungaji wa bao pekee la Real Madrid alilazimika kutolewa uwanjani katika dakika ya 67 ya mchezo na kukimbizwa hospitalini baada ya kugongana kwa bahati mbaya na mchezaji mwenzake wa Real Madrid,Toni Kroos.

    Taarifa iliyochapishwa kwenye mtandao wa Real Madrid imesema kuwa baada ya mlinzi huyo kufanyiwa vipimo kwenye hospitali ya chuo kikuu cha Sanitas La Moraleja imebainika kuwa amevunjika mbavu mbili.Mbavu ya saba na ya nane. 
    Taarifa hiyo imeongeza kuwa kurejea tena dimbani kwa mlinzi huyo wa zamani wa Porto kutategemea sana kasi ya uponaji wa majeraha hayo.


    Hii ina maana kuwa Pepe atakosa michezo yote ya robo fainali ya klabu bingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich pamoja wa mchezo wa El Classico dhidi ya Barcelona Aprili 23 mwaka huu.

    Kuumia kwa Pepe ni pigo jingine kubwa kwa Real Madrid ambayo hivi karibuni ilimpoteza mlinzi wake mahiri Mfaransa,Raphael Varane aliyepata jeraha la nyama za paja.



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Pepe aipa pigo Real Madrid Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top