728x90 AdSpace

  • Latest News

    Sunday, April 09, 2017

    Barca hoi Hispania,yagongwa 2-0 La Liga,Neymar ala umeme


    Malaga,Hispania.

    BARCELONA imeshindwa kuwang'oa kileleni mahasimu wao wakubwa kwenye mbio za ubingwa wa La Liga,Real Madrid baada ya usiku huu kukubali kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Malaga kwenye dimba la ugenini la Estadio La Rosaleda.

    Awali kulikuwa na hofu kuwa Barcelona ingeipiku Real Madrid kileleni baada ya mapema kulazimishwa sare ya bao 1-1 na Atletico Madrid huko Santiago Bernabeu lakini mabao mawili ya dakika za 32 na 90 ya Sandro Ramirez na Jony yametosha kuiduwaza miamba hiyo ya Camp Nou.


    Aidha katika mchezo huo ilishuhudiwa Barcelona ikilazimika kumaliza mchezo ikiwa na wachezajo kumi uwanjani baada ya Neymar kutolewa uwanjani kwa kadi mbili za njano katika dakika ya 66 kwa mchezo mbaya dhidi ya Diego Llorente.

    Kichapo hicho kimeiacha Barcelona ikibaki kwenye nafasi yake na pointi zake 69.Pointi tatu nyuma ya Real Madrid yenye pointi 72 na mchezo mmoja mkononi.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Barca hoi Hispania,yagongwa 2-0 La Liga,Neymar ala umeme Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top