728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, April 08, 2017

    Madrid dabi yakosa mbabe,yaisha sare ya 1-1


    Madrid,Hispania.

    REAL MADRID imeshindwa kupata ushindi wake wa kwanza nyumbani dhidi ya wapinzani wao wakubwa, Atletico Madrid baada ya muda mfupi uliopita kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 katika mchezo mkali wa ligi ya La Liga uliochezwa huko Santiago Bernabeu.

    Pepe ndiye aliyekuwa wa kwanza kuleta tofauti kwenye mchezo huo baada ya kuifungia Real Madrid bao la kuongoza katika dakika ya 52 kwa kichwa akiunganisha mpira wa krosi uliopigwa na Toni Kroos.


    Bao hilo lilidumu mpaka dakika ya 85 ya mchezo kabla ya mshambuliaji Mfaransa,Antoine Griezmann kuisawazishia Atletico Madrid baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Andre Corre na kupiga mpira uliotinga kulia kwa kipa wa Real Madrid, Keylor Navas na kufanya mchezo huo uishe kwa sare ya bao 1-1.

                                 

    Vikosi

    Real Madrid: Navas, Carvajal, Pepe, Ramos,Marcelo, Casemiro, Kroos, Modric, Bale,Ronaldo and Benzema

    Atletico Madrid: Oblak, Juanfran, Savic,Godin, Luis, Koke, Fernandez, Niguez,
    Carrasco, Torres, Griezmann





    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Madrid dabi yakosa mbabe,yaisha sare ya 1-1 Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top