728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, April 08, 2017

    Yanga SC safi shirikisho,yawazaba Waalgeria 1-0 U/Taifa


    Dar Es Salaam,Tanzania.

    MABINGWA wa ligi kuu Tanzania bara,Yanga SC leo wameutumia vyema Uwanja wa Taifa,Dar Es Salaam baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya MC Alger ya Algeria katika mchezo wa kwanza wa hatua ya kuwania tiketi ya kutinga hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.


    Bao pekee la mchezo huo limefungwa na kiungo wa kimataifa wa Zimbabwe,Thabani Kamusoka katika dakika ya 60 baada ya kazi nzuri ya Mnyarwanda,Haruna Niyonzima Fabregas.

    Timu hizo zitarudiana tena Jumamosi ijayo huko Alger,Algeria na timu itakayopata ushindi mkubwa itafuzu hatua ya makundi.


    Yanga SC leo iliwakilishwa na

    1. Deogratius Munishi 
    2. Hassani Kessy
    3. Haji Mwiji
    4. Nadir Haroub
    5. Vicent Bossou 
    6. Juma Saidi 
    7. Saimoni Msuva 
    8. Thabani Kamusoko 
    9. Obrey Chirwa 
    10. Haruna Niyonzima 
    11. Deusi Kaseke/Donald Ngoma 



    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Yanga SC safi shirikisho,yawazaba Waalgeria 1-0 U/Taifa Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top