728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, April 08, 2017

    Giggs aitaka Man United kuwa kama Liverpool




    Cairo,Misri.

    WINGA wa zamani wa Mashetani Wekundu wa Manchester United,Ryan Giggs ameitaka klabu yake hiyo ya zamani kuiga mfano wa wapinzani wao Liverpool katika upachikaji mabao.

    Giggs ameyasema hayo akiwa nchini Misri alipokwenda kwenye ziara ya kulitembeza kombe la klabu bingwa Ulaya inayojulikana kama Heineken Champions League Trophy Tour.

    Giggs ambaye kwa sasa anafanya kazi ya uchambuzi wa masuala ya soka kwenye Televisheni za Uingereza ameitaka Manchester United kuacha kumtegemea  zaidi Zlatan Ibrahimovic katika upachikaji mabao na badala yake mabao yawe yanapatikana kutoka pande zote za uwanja kama wafanyavyo Liverpool.Tofauti na hali ilivyo sasa,Ibrahimovic akikosekana na mabao yanakosekana.

    Nyota huyo raia wa Wales anapingana na mashabiki wa klabu hiyo ambao wanaoamini kuwa kushindwa kufunga mabao ya kutosha kwa Manchester United kunasababishwa na kukosa bahati pamoja na makosa ya kizembe ya waamuzi wanaochezesha michezo ya klabu yao.



    Mabao yanapaswa kupatikana kutoka kila pande za uwanja.Hivyo ndiyo Manchester United yetu ilivyokuwa.Ningefunga mabao saba au manane,Becks hivyo hivyo,Scholes pia.Washambuliaji wote wanne wa mbele.Mabeki wa kati.Denis Irwin pia.Mabao alipatikana kutoka kila pande za uwanja.


    Huwezi kumtegemea mtu mmoja pekee kwa sababu anaweza akawa hayuko fiti ama hayuko kabisa mchezoni.Leceister City msimu uliopita ilikuwa sawa. Jamie Vardy alifunga mabao mengi na Riyad Mahrez akafunga 17.Hicho ndicho unachohitaji.
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Giggs aitaka Man United kuwa kama Liverpool Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top