728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, April 08, 2017

    Mbaraka Yusuph kumfuata Samatta


    Faridi Miraji , Dar es salaam.                        

    MCHEZAJI bora wa mwezi wa tatu wa ligi kuu ya Vodacom,Mbaraka Yusuph kuna uwezekano msimu ujao tukamuona kwenye vilabu vikubwa vya Simba,Yanga, Azam au nje ya nchi.

    Mbaraka ambaye Kwa sasa yuko kwenye kiwango cha hali ya juu akiwa amefunga magoli kumi na moja kwenye ligi kuu,mkataba wake unaisha mwisho wa msimu kuna uwezekano wa kusajiliwa na vilabu vikubwa .

    Mbaraka Alisema "Ni  kweli mkataba wa mwaka mmoja niliosaini na timu yangu ya Kagera Sugar unamalizika mwisho wa msimu,  kuna timu nyingi zinanihitaji  ila sitaziweka wazi Kwa sasa mpaka mwisho wa msimu , ila malengo yangu ni kwenda kucheza nje ya nchi. 

    Pia Mbaraka amesema Siri ya mafanikio yake ni kujituma na kufanya mazoezi Kwa sana Kwa sasa anafanya mazoezi Mara mbili Kwa siku asubuhi na jioni na pia huenda gym.

    Mbaraka ambaye anawindwa ni vilabu vikubwa vya Simba,  Yanga na Azam Kwa sasa anatamani ndoto yake itimie ya kucheza nje ya nchi, Hii Itakuwa fulsa kwake na faida Kwa taifa letu kama kweil ataamua Kufuata nyayo za Mbwana Ally Samatta,  Umri wake Bado mdogo ni muda mwafaka kwake kutoka nje ya Nchi. 

    Mbaraka Yusuph Ambaye alikuwa na mgogoro wa kimkataba na timu yake ya zamani ya Simba baada ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja na Kagera sugar. Simba walimuwekea Pingamizi Kwa  Shirikisho la Mpira wa miguu Tanzania (TFF) wakidai Bado walikuwa na mkataba wa mwaka mmoja aliosaini akiwa na timu ya Vijana ya Simba.

    Lakini Tff waliwaambia  Kagera Sugar  na Simba wakutane walimalizane vizuri nje ya kamati.  Yanayosemekana Simba na Kagera hawakumalizana ndio maana juzi Simba walikuwa wanalalamika Kagera sugar kumchezesha Mbaraka wakidai ni mchezaji Wao. 
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Mbaraka Yusuph kumfuata Samatta Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top