Manchester,England.
JUZI Alhamisi staa wa
England,Jesse Lingard alisaini mkataba mpya wa miaka minne wa kuendelea kusalia
klabuni Manchester United.
Lingard mwenye umri wa
miaka 24 amezawadiwa mkataba huo mnono utakaodumu mpaka mwaka 2021 baada ya kuonyesha
kiwango bora katika misimu miwili iliyopita.Mkataba huo mpya umeripotiwa kuwa
utakuwa ukimwingizia Lingard mshahara wa Paundi 100,000 kwa wiki.Mara tatu
zaidi ya ule wa awali wa Pauni 30,000 kwa wiki.
Mshahara huo mpya
umemfanya Lingard aingie kwenye orodha ya nyota wanaovuta mkwanja mrefu zaidi
klabuni Manchester United mbele ya mastaa kama Michael Carrick,Erick Bailly na
Antony Martial.
Ifuatayo ni orodha wa
wachezaji wanaovuta mshahara mrefu zaidi kalabuni Manchester United
1.
Wayne Rooney: £300,000/w
2.
Paul Pogba: £290,000/w
3.
Zlatan Ibrahimovic: £220,000/w
4.
David De Gea: £200,000/w
5.
Henrikh Mkhitaryan: £180,000/w
6.
Juan Mata: £145,000/w
7.
Marouane Fellaini: £120,000/w
8.
Phil Jones: £120,000/w
9.
Chris Smalling: £120,000/w
10.Luke
Shaw: £100,000/w
11.Jesse
Lingard: £100,000/w
12.Michael
Carrick: £80,000/w
13.Eric
Bailly: £75,000/w
14.Anthony
Martial: £70,000/w
15.Marcus
Rashford: £35,000/w
0 comments:
Post a Comment