728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, April 05, 2017

    Azam FC yaidunda Ndanda FC na kuzifuata Simba,Mbao nusu fainali FA Cup


    Paul Manjale,Dar Es Salaam.

    AZAM FC imefanikiwa kuungana na vilabu vya Simba na Mbao FC kutinga nusu fainali ya michuano ya kombe la Azam Sports Federation Cup maarufu kama FA Cup baada ya usiku huu kuifunga Ndanda FC ya mkoani Mtwara mabao 3-1 katika mchezo mkali wa robo fainali ya tatu uliochezwa kwenye Uwanja wa Chamazi,Mbande nje kidogo ya jiji la Dar Es Salaam.

    Mabao ya Azam FC Shabani katika mchezo wa leo yamefungwa na mshambuliaji kinda, Shabani Iddi aliyefunga mabao mawili katika dakika za 13 na 45 huku bao la tatu likitiwa kimiani na winga machachari,Ramadhani Singano Messi katika dakika ya 46.Bao la kufutia machozi la Ndanda FC limefungwa na William Lucian katika dakika ya 14 ya kipindi cha kwanza.

    Aidha katika mchezo huo timu hizo zililazimika kufanya mabadiliko ya lazima kutokana na wachezaji wao wa kutumainiwa kuumia.Ndanda ilimpoteza kipa wake Jeremiah Kisubi aliyeumia na nafasi yake kuchukuliwa na Wilbert Mweta.Azam FC wao ilimpoteza Yakubu Mohamed aliyeumia na nafasi yake kuchukuliwa na David Mwantika. 

    Mbali ya Azam FC timu nyingine ambazo tayari zimeshakata tiketi ya kucheza nusu fainali ya michuano ya kombe hilo ni Simba SC iliyoitoa Madini FC ya Arusha.Nyingine ni Mbao FC iliyoitoa Kagera Sugar.Robo fainali ya nne itakuwa kati ya mabingwa Yanga SC watakaoikaribisha Tanzania Prisons Aprili 22 mwaka huu.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Azam FC yaidunda Ndanda FC na kuzifuata Simba,Mbao nusu fainali FA Cup Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top