728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, April 10, 2017

    TP Mazembe yavuna ushindi mubashara kombe la shirikisho Afrika


    Lubumbashi, DR Congo.

    TP Mazembe imeendelea vyema na kampeni zake za kuhakikisha kuwa inafuzu hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho Afrika baada ya Jumapili jioni kuwatungua Waarabu wa Algeria,JS Kabylie kwa mabao 2-0 huko Lubumbashi.

    Ikicheza kwenye dimba lake la Stade de Lubumbashi, TP Mazembe ilijipatia mabao yake kupitia kwa Mzambia,Nathan Sinkala na mlinzi wa Mali,Salif Coulibaly.

    Timu hizo zitarudiana tena Jumapili ijayo huko Stade
    du Tizi-Ouzou huko Algeria ambapo timu itakayopata ushindi mkubwa wa jumla itakuwa imefuzu hatua ya makundi ambayo inatarajiwa kuanza mwezi ujao.


    Matokeo mengine ya michezo ya kombe la shirikisho Afrika.Club Africain ya Tunisia ikiwa ugenini Curepipe imechomoza na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Port Louis ya Mauritia.

    Enugu Rangers ya Nigeria ikiwa nyumbani Enugu imelazimishwa sare ya mabao 2-2 na Zesco United ya Zambia.Tanda ya Ivory Coast imeifunga Platinum Stars ya Afrika Kusini mabao 2-0.

    Matokeo Kamili

    Port Louis (Mauritius) 1-2 Club Africain (Tunisia)
    TP Mazembe (DR Congo, holders) 2-0 JS Kabylie (Algeria)
    Enugu Rangers (Nigeria) 2-2 Zesco United (Zambia)
    Tanda (Ivory Coast) 2-0 Platinum Stars (South Africa)


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: TP Mazembe yavuna ushindi mubashara kombe la shirikisho Afrika Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top