728x90 AdSpace

  • Latest News

    Monday, April 10, 2017

    Kocha wa zamani wa Simba SC atupiwa virago Ghana.



    Kumasi,Ghana.

    KLABU ya Asante Kotoko ya Ghana imemtupia virago aliyekuwa kocha wake mkuu Mcroatia,Zradvko Logarussic kwa kile kinachodaiwa kuwa ni mfululizo wa matokeo mabaya kwenye ligi kuu ya nchi hiyo.

    Logarussic aliyewahi kuvifunza kwa nyakati tofauti vilabu vya Simba SC ya Tanzania na Gor Mahia ya Kenya ametupiwa virago muda mfupi baada ya jana Jumapili kuiongoza Asante Kotoko kulazimishwa sare ya bila kufungana na Ebusua Dwarfs nyumbani Kumasi.

    Taarifa iliyotolewa Asante Kotoko imesema uwamuzi huo umefikiwa katika kikao cha dharura cha wakuu wa klabu hiyo kilichoketi muda mfupi baada ya kumalizika kwa mchezo wao dhidi ya Ebusua Dwarfs na kuamua kuachana na kocha huyo aliyehudumu kwa miezi mitatu tu.

    Ikumbukwe mapema wiki iliyopita mashabiki wenye hasira wa Asante Kotoko walivamia kwenye uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo wakimtaka Logarussic abwage manyanga kuwafundisha mabingwa hao mara mbili wa Afrika.

    Logarussic alijiunga na Asante Kotoko Januari 10 mwaka huu.Mpaka anatimuliwa alifanikiwa kuiongoza klabu hiyo kucheza michezo 11akishinda michezo mitano,akitoka sare michezo minne na kufungwa michezo miwili.





    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Kocha wa zamani wa Simba SC atupiwa virago Ghana. Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top