728x90 AdSpace

  • Latest News

    Wednesday, April 05, 2017

    Simba SC yafanya mauaji kanda ya ziwa,yainyuka Geita 8-0 kirafiki,Blagnon apiga hat-trick


    Geita,Mwanza.

    IKIWA na kumbukumbu mbaya ya kufungwa mabao 2-1 na Kagera Sugar kwenye mchezo wake uliopita wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara,Simba SC leo imechomoza makucha yake na kuisasambua vikali Geita Gold FC kwa kuifunga mabao 8-0 katika mchezo safi wa kirafiki uliochezwa jioni ya leo kwenye Uwanja wa shule ya msingi Waja huko wilayani Geita mkoani Mwanza.

    Shujaa wa Simba SC katika mchezo wa leo alikuwa ni mshambuliaji wa kimataifa wa Ivory Coast,Friedrich Blagnon aliyepachika wavuni mabao matatu (hat-trick).

    Mabao mengine ya Simba SC yamefungwa na Mohammed Ibrahim aliyefunga mabao mawili.Juma Liuzio,Said Ndemla na Mwinyi Kazimoto wamefunga bao moja kila mmoja.





    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: Simba SC yafanya mauaji kanda ya ziwa,yainyuka Geita 8-0 kirafiki,Blagnon apiga hat-trick Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top