728x90 AdSpace

  • Latest News

    Tuesday, June 07, 2016

    YANGA SC YAMTUPIA VIRAGO ISSOUFOU BOUBACAR,TWITE ALAMBA DILI JIPYA

    Dar es Salaam,Tanzania.

    YANGA SC leo imemtupia virago aliyekuwa winga wake Issoufou Boubacar Garba toka Niger ikiwa ni miezi sita tu tangu imsajili kwa mbwembwe kuchukua nafasi wa winga Mbrazil Andres Coutinho.

    Boubacar ametupiwa virago kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kushindwa Kuonyesha makali yake kama ilivyotarajiwa hali iliyopelekea awe ni mchezaji wa kukaa benchi kila uchao.

    Kabla ya kutua Yanga SC Boubacar aliwahi kuwa na vilabu vya Tunisia vya Club Africain na ES Hammam-Sousse ambavyo hakubahatika hakuvichezea.

    Wakati huohuo Yanga SC imempa mkataba mpya wa miaka miwili kiungo/beki wake Mnyarwanda Mbuyu Twite.Hii ina maana kwamba Twite ataendelea kuwa mali ya wanajangwani hao mpaka mwaka 2018.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: YANGA SC YAMTUPIA VIRAGO ISSOUFOU BOUBACAR,TWITE ALAMBA DILI JIPYA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top