Milan,Italia.
CHAMA cha soka cha Italia (FIGC) leo kimemtangaza Giampiero Ventura kuwa Kocha Mkuu mpya wa timu ya taifa hilo akichukua nafasi ya kocha wake wa sasa Antonio Conte ambaye anatarajiwa kujiunga na Chelsea mara baada ya kuisha kwa michuano ya Ulaya [Euro 2016] hapo mwezi Julai 10.
Ventura,68,amepewa kibarua hicho kikubwa zikiwa zimepita siku chake tu tangu atangaze kuachana na klabu ya Torino na jukumu lake la kwanza litakuwa ni kuhakikisha Italia inafuzu fainali za kombe la dunia la mwaka 2018 zitakazoandaliwa nchini Urusi. Italia iko kundi G pamoja na mataifa ya Hispainia, Albania,Israel, Macedonia na Liechtenstein.
Ventura alijiunga na Torino Juni 2011.Kabla ya hapo alikuwa akihudumu katika vilabu vya Bari, Pisa, Verona, Messina, Napoli,Cagliari, Udinese na Sampdoria.
0 comments:
Post a Comment