728x90 AdSpace

  • Latest News

    Thursday, June 09, 2016

    MAHAKAMA YAAMURU NYOTA WA CHELSEA ALIYEKO TANZANIA AKAMATWE MARA MOJA

    Glasgow,Scotland.

    MAHAKAMA ya Glasgow’s Justice of the Peace Court ,ya Scotland imetoa hati kwa wanausalama wa nchi hiyo kumkamata na kumfikisha mahakamani hapo kinda wa Chelsea ya England,Islam Feruz,kujibu mashitaka matatu yanayomkabili.

    Hati hiyo imetolewa na muendesha mashitaka wa mahakama hiyo Frances McCartney baada ya Ferouz,20, kushindwa kufika mahakamani hapo wakati kesi yake iliipoanza kusikilizwa jana Jumatano Juni 8,2016 kwa kile kinachodaiwa kuwa nyota huyo mwenye asili ya Somalia yuko nchini Tanzania akifanya mazoezi.

    Ferouz anakabiliwa na makosa matatu ambayo ni kuendesha gari lake la kifahari aina ya Porsche lenye thamani ya £80,000 wakati akijua fika kuwa amezuiwa.

    Kosa la pili aliwadanganya maafisa wa polisi waliomkamata kwa kuwaambia kuwa anaitwa Saeed Cabadalla.Kosa la tatu ni kuendesha gari bila ya kuwa na leseni.

    Ferouz alijiunga na Chelsea mwaka 2014 akitokea Celtic ya Scotland.


    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAHAKAMA YAAMURU NYOTA WA CHELSEA ALIYEKO TANZANIA AKAMATWE MARA MOJA Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top