Brondby,Denmark
MLINZI wa zamani wa Liverpool na timu ya taifa ya Dermark Daniel Agger,31, rasmi leo ameachana na mchezo wa soka.
Agger ambaye atakumbukwa kwa mashuti yake makali makali ametangaza uamuzi huo kupitia ukurasa wake wa twitter ikiwa ni misimu miwili tu tangu arejee katika klabu yake ya utotoni ya Brondby mwaka 2014 akitokea Liverpool kwa ada ya £3m.
Katika kipindi cha miaka miwili alichokuwa na Brondby,Agger alifanikiwa kutwaa mara mbili mfululizo tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa Ligi kuu ya Dermark.Pia akifanikiwa kutwaa ubinga wa Ligi ya Dermark mara moja pamoja na vikombe viwili vya Ligi.
Akiwa na Liverpool Agger aliyefanikiwa kuichezea michezo 232 na kuifungia mabao 14 katika kipindi cha miaka minane alichodumu Anfield.
Sababu kubwa ya kufikia uamuzi huo imedaiwa kuwa ni majeraha ya mara kwa mara ambayo yamekuwa yakimpata nyota huyo.
0 comments:
Post a Comment