Philadelphia,Marekani.
URUGUAY ikicheza kwa mara ya pili bila ya staa wake Luis Suarez, imetupwa nje ya michuano ya Copa America Centenario baada ya alfajiri ya leo kufungwa bao 1-0 na Venezuela katika mchezo mkali wa Kundi C uliochezwa katika uwanja wa Lincoln Financial Field huko Philadelphia,Marekani.
Bao pekee la mchezo huo limefungwa dakika ya 36 ya kipindi cha kwanza na mshambuliaji wa West bromwich Albion,Jose Solomon Rondon.Kwa matokeo hayo Venezuela imetinga robo fainali baada ya kufikisha pointi sita baada ya kushuka dimbani mara mbili.
Uruguay wao wametupwa nje ya mashindano hayo baada ya kushindwa kupata pointi yoyote katika michezo miwili ambayo wameshacheza mpaka sasa.Katika mchezo wa kwanza Uruguay walifungwa mabao 3-1 na Mexico.
VIKOSI
Uruguay (4-4-2) : Muslera; M. Pereira,Gimenez, Godin, G. Silva; Sanchez, Arevalo,Ramirez, Alvaro; Stuani,Cavani
Venezuela (4-2-3-1): Hernandez; Rosales,Angel, Vizcarrondo,Feltscher; Rincon,Figuera; Martinez, Guerra, Penaranda;Rondon
0 comments:
Post a Comment