728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 21, 2016

    WABABE WA YANGA SC KLABU BINGWA AFRIKA AL AHLY WAICHAPA AS ROMA ILIYOKUWA NA TOTTI,DZEKO NA SALAH

    Al-Ain,UAE.

    Klabu ya Al Ahly ya Misri imeonyesha kuwa siyo timu ya mzaha mzaha baada ya Ijumaa Usiku kuibuka na Ushindi mkubwa wa mabao 4-3 dhidi ya AS Roma ya Italia katika mchezo mkali wa Kimataifa wa Kirafiki Uliochezwa katika uwanja wa Hazza Ben Zayed huko UAE.

    Al Ahly ambayo mwezi Aprili iliitupa Yanga SC ya Tanzania nje ya michuano ya Vilabu Bingwa Afrika,ilikuwa ya kwanza kupata bao la kuongoza dakika ya 13 kupitia kwa mshambuliaji wake Mghana John Antwi.Antwi alifunga bao hilo baada ya kupokea pasi nzuri toka kwa Moemen Zakareya.


    Kuingia kwa bao hilo kuliiamsha AS Roma ambayo ilikuja juu na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 20 kupitia kwa mshambuliaji wake Edin Dzeko.Dzeko alifunga bao hilo baada ya kupokea pasi ndefu toka kwa nahodha Francesco Totti na kuwalamba chenga walinzi wawili wa Al Ahly,Rami Rabia na Mohamed Naguib na kisha kufumua mkwaju mkali uliomshinda mlinda mlango Sherif Ekramy.

    Zakareya akimtoka Kevin Strotmann

    Dakika ya 41 Mohammed Salah aliipa uongozi AS Roma baada ya kuifungia bao la pili akitumia makosa ya mlinzi Rami Rabia aliyeshindwa kuuondosha mpira uliopigwa na Edin Dzeko.Lakini sekunde chache klabu ya mapumziko Moemen Zakareya aliifungia Al Ahly bao la kusawazisha na kufanya timu ziende ziende mapumziko zikiwa nguvu sawa.

    Mabao mengine katika mchezo huo kwa upande wa Al Ahly yamefungwa na Walid Soliman (54) pamoja na Ahmed El-Sheikh (94) huku lile la AS Roma likifungwa na William Vainqueur (90).

    Hii ni mara ya tatu kwa miamba hiyo kukutana, mara ya kwanza ilikuwa ni 2002 na Al Ahly kushinda kwa mabao 2-1,mwaka 2008 AS Roma iliishinda kwa mabao 3-0.j
    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: WABABE WA YANGA SC KLABU BINGWA AFRIKA AL AHLY WAICHAPA AS ROMA ILIYOKUWA NA TOTTI,DZEKO NA SALAH Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top