728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 21, 2016

    SERENGETI BOYS DIMBANI TENA LEO INDIA,INASAKA KUTINGA FAINALI

    Goa,India.

    Timu ya Taifa ya Vijana ya Tanzania walio chini ya umri wa miaka 17 "Serengeti Boys" leo jioni itashuka tena dimbani Tilak Maidan huko Goa,India kuvaana na Timu Taifa ya Vijana ya Malaysia katika muendelezo wa michezo ya Vijana ya AIFF Youth Cup,2016.

    Serengeti Boys ambayo iko kileleni mwa msimamo wa michuano hiyo baada ya kujikusanyia pointi tano katika michezo mitatu,hivyo inahitaji ushindi wowote ule katika mchezo wa leo ili iweze kucheza fainali hapo siku ya Jumatano Mei 25.Malaysia ina pointi moja baada ya kucheza michezo miwili.

    Katika mchezo mwingine utakaochezwa leo,Marekani itaumana na Korea Kusini.Marekani na Korea Kusini zote zina pointi nne kila moja baada ya kushuka dimbani mara mbili.Hivyo mchezo huo unatarajiwa kuwa wa vuta nikuvute kwani timu yoyote itakayoshinda leo itaingia fainali.

    Michezo hiyo itaendelea tena Mei 23,2016

    Malaysia v Marekani
    Uwanja:Tilak Maidan Stadium , Goa

    Mei 23,2016

    Korea Kusini v India
    Uwanja:Tilak Maidan Stadium , Goa

    Mei 25,2016

    Kumsaka Mshindi wa Tatu na wa Nne

    Fainali.

    Mshindi wa kwanza wa kundi v Mshindi wa pili wa kundi

    Uwanja:Tilak Maidan Stadium , Goa...

    MSIMAMO ULIVYO

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: SERENGETI BOYS DIMBANI TENA LEO INDIA,INASAKA KUTINGA FAINALI Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top