728x90 AdSpace

  • Latest News

    Saturday, May 21, 2016

    MAZZARRI KOCHA MPYA WATFORD

    Watford,England.

    Klabu ya Watford yenye makao yake makuu katika dimba la Vicarage Road imemtangaza Muitaliano Walter Mazzarri kuwa Kocha wake Mkuu mpya kwa mkataba wa miaka mitatu.

    Mazzarri,54 mwenye uzoefu mkubwa na mbinu nyingi za kufundisha mpira amesaini kuchukua mikoba iliyoachwa na Kocha Muhispania Quique Sanchez Flores aliyesitishiwa mkataba wake mapema wiki iliyopita.

    Mazzarri aliyewahi kuvinoa vilabu vya Sampdoria, Napoli na Inter Milan anakuwa kocha wa nane kujiunga na Watford tangu Klabu hiyo ilipochukuliwa rasmi na familia ya Pozzo mwaka 2012.

    Kocha huyo amekuwa nje ya dimba tangu alipoachana na Inter Milan mwaka 2014.

    • Blogger Comments
    • Facebook Comments

    0 comments:

    Post a Comment

    Item Reviewed: MAZZARRI KOCHA MPYA WATFORD Rating: 5 Reviewed By: Unknown
    Scroll to Top