Warsaw,Poland.
Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Poland Adam Nawalka ametangaza kikosi cha wachezaji 28 ambacho kitapunguzwa na kubakia na wachezaji 23 watakaoiwakilisha nchi hiyo katika michuano ya Ulaya [Euro 2016] itakayofanyika nchini Ufaransa kuanzia Juni 10 na kufikia tamati Julai 10.
Katika kikosi hicho cha awali Nawalka amewatema wakongwe Sebastian Mila (Lechia Gdansk) na Lukasz Szukala (Osmanslispor) na kumjuisha kwa mara ya kwanza kinda wa Benfica ya Ureno Pawel Dawidowicz,20.Nahodha Robert Lewandowski pia amejumuishwa.
Kikosi hicho cha wachezaji 28 kitakutana kwa ajili ya kuweka kambi ya muda mfupi kabla ya kupunguzwa na kubaki 23 baada ya kucheza michezo miwili ya kimataifa dhidi ya Uholanzi Juni, 1 huko Gdansk na Lithuania siku tana baadae huko Krakow.
Poland iko kundi E pamoja na mataifa ya Ujerumani,Ukraine na Ireland ya Kaskazini.Poland itacheza mchezo wake wa kwanza kwa kuvaana Ireland ya Kaskazini huko Nice Juni, 12,kabla ya kusafiri mpaka Paris kucheza na Ujerumani siku nne baadae.Poland itacheza mchezo wake wa mwisho wa hatua ya makundi kwa kuvaana na Ukraine katika uwanja wa Stade Veledrome huko Marseille Juni, 21.
KIKOSI CHA AWALI NI:
Makipa: Artur Boruc (Bournemouth/ENG), Lukasz Fabianski (Swansea City/ENG), Wojciech Szczesny (Roma/ITA),Przemyslaw Tyton (VfB Stuttgart/GER)
Mabeki: Thiago Cionek (Palermo/ITA),Pawel Dawidowicz (Benfica/POR), Kamil Glik (Torino/ITA), Artur Jedrzejczyk,Michal Pazdan (both Legia Warsaw),Lukasz Piszczek (Borussia Dortmund/GER), Bartosz Salamon (Cagliari/ITA),Jakub Wawrzyniak (Lechia Gdansk)
Viungo: Jakub Blaszczykowski (Fiorentina/ITA), Kamil Grosicki (Rennes/FRA), Tomasz Jodlowiec (Legia
Warsaw), Bartosz Kapustka (Cracovia),Grzegorz Krychowiak (Sevilla/ESP),Karol Linetty (Lech Poznan), Krzysztof Maczynski (Wisla Krakow), Slawomir Peszko (Lechia Gdansk), Maciej Rybus (Terek Grozny/RUS), Filip Starzynski (Zaglebie Lubin), Pawel Wszolek (Hellas Verona/ITA), Piotr Zielinski (Empoli/ITA)
Washambuliaji: Robert Lewandowski (Bayern Munich/GER), Arkadiusz Milik (Ajax/NED), Artur Sobiech (Hanover/GER), Mariusz Stepinski (Ruch Chorzow)
0 comments:
Post a Comment