Paris,Ufaransa.
Mshambuliaji wa Paris Saint Germain Msweden Zlatan Ibrahimovic ameibuka kinara baada ya kutangazwa mchezaji bora wa mwaka wa Ligi daraja la Kwanza Ufaransa "Ligue 1" kwa msimu wa tatu mfululizo katika kipindi cha miaka minne.
Ibrahimovic,34 ametwaa tuzo hiyo baada ya kuwashinda Ángel Di María wa Paris Saint-Germain ,Hatem Ben Arfa wa OGC Nice wa Lassana Diarra wa Olympique de Marseille
"Ikumbukwe msimu huu Ibrahimovic amefunga mabao 35 Ligue 1 na 45 katika michezo yote na kuiwezesha Paris Saint Germain kutwaa mataji mawili.Ligue 1 na taji la ligi (France Cup)".
Tuzo ya golikipa bora wa mwaka wa Ligue 1 imeenda wa Steve Mandanda wa Olympique de Marseille,31.Hii imekuwa ni tuzo yake ya nne akitwaa mwaka 2008, 2011,2015 na 2016.
Tuzo ya mchezaji bora kijana imeenda kwa Ousmane Dembélé wa Stade Rennais FC aliyewashinda Vincent Koziello wa Nice,Thomas Lemar wa AS Monaco na Adrien Rabiot wa Paris Saint-Germain.
ORODHA YA WASHINDI
LIGUE 1
* Mchezaji bora wa mwaka wa Ligue 1 - Zlatan Ibrahimovic (Paris Saint-Germain)
* Mchezaji bora kijana wa mwaka wa Ligue 1 - Ousmane Dembélé (Rennes)
* Goli bora la mwaka la Ligue Pierrick Capelle (Angers SCO v EA Guingamp)
* Kocha bora wa mwaka wa Ligue 1 - Laurent Blanc (Paris Saint-Germain)
* Goli Kipa bora wa mwaka wa Ligue 1 - Steve Mandanda (Marseille)
0 comments:
Post a Comment