Barcelona,Hispania.
Bila shaka Mruguayi Luis Suarez,29 ndiye mshambuliaji bora kwa sasa dunia.
Ziko takwimu nyingi za kuthibisha ubora huo.Ila chache kati ya hizo ni kuwa msimu huu Suarez amefunga mabao 37 katika michezo 34 ya La Liga.Mabao manne zaidi ya Cristiano Ronaldo na kumi na moja zaidi ya Lionel Messi.
Jumla amefunga mabao 56 katika michezo 51ya michuano mbalimbali kwa ngazi ya klabu.
AONGOZA KWA MABAO ULAYA
Katika Ligi zote kubwa Suarez ndiyo kinara wa upachikaji mabao!! Suarez anaongoza akiwa amepachika mabao 37 nafasi ya pili inashikwa na Cristiano Ronaldo mwenye mabao 33,nafasi ya tatu imeshikwa na mshambuliaji wa Benfica Jonas mwenye mabao 31.
AFIKISHA MABAO 301
Mabao mawili aliyoyafunga Luis Suarez Jumapili na kuiwezesha Barcelona kuichapa Espanyol kwa jumla ya mabao 5-0 yamemfanya mshambuliaji huyo wa zamani wa Liverpool afikishe mabao 301 tangu alipoanza kucheza soka la kulipwa.
Chini ni idadai ya mabao na vilabu alivyochezea
Nacional-12
Groningen -15
Ajax - 111
Liverpool - 82
Barca - 81
AFUNGA MABAO MENGI ZAIDI YA VILABU VITANO VYA HISPANIA NA KIMOJA CHA ENGLAND.
Kitu kingine cha ajabu zaidi ni kuwa Suarez amefunga mabao mengi zaidi ya vilabu sita,vitano vya Hispania na kimoja cha England.
Timu Mabao
Aston Villa - 11
Espanyol - 36
Levante - 36
Getafe - 36
Malaga - 34
Real Betis - 32
Suarez - 37.
0 comments:
Post a Comment