KATISHA.Hii ndiyo kauli pekee unayoweza kuitumia kumuelezea Cris Scott shabiki wa kutupwa wa Manchester United ambaye ameonyesha mapenzi aliyonayo kwa klabu hiyo kwa kutumia miezi mitatu akiujenga uwanja wa Old Trafford unaomilikiwa na maimba hiyo ya ligi kuu England kwa kutumia njiti za viberiti.
Scott,41 ametumia masaa 450,katika siku 19 nzima katika kipindi cha miezi mitatu akiifanya kazi hiyo ambayo ilimfanya hata asipate muda wa kuitazama klabu yake siku ya jumapili ilipokuwa ikimenyana na Arsenal na kuambulia kichapo cha magoli 3-0.
Pia katika kuutia naksi uwanja huo Scott amejenga pia sanamu la Alex Ferguson kama linavyoonekana katika uwanja halisi wa Old Trafford.
0 comments:
Post a Comment