Mwanamitindo wa Ukraine amefanya tukio kubwa na la aina yake baada ya kuamua kupiga picha za utupu ili kuiikoa timu yake inayokabiliwa na hali mbaya ya kiuchumi.
Mrembo huyo anayeitwa Angelina Petrova anatokea Zaporizhia kusini mashariki mwa Ukraine katika mkoa wa Zaporizhia Oblast aliamua kufanya tukio hilo baada ya timu ya mtaani kwake ya FC Metalurh Zaporizhya kuanza kufirisika na kuwa mbioni kupotea katika ramani ya soka.
Angelina ili kuonyesha mapenzi na timu hiyo aliamua kupiga picha hizo katika uwanja wa nyumbani wa timu hiyo inayoshiriki ligi ya Ukraine.Mpaka sasa FC Metalurh Zaporizhya inaburuza mkia ikiwa imejikusanyia jumla ya pointi 3 katika michezo 8.
Taarifa kutoka Ukraine zinasema FC Metalurh Zaporizhya imeanza kuziuza picha za utupu za Angelina na tayari mafanikio yameshaanza kuonekana kwani watu wanazichangamkia kwa kasi ya ajabu.
0 comments:
Post a Comment