Barcelona,Hispania.
Unalikumbuka lile sakata la Lionel Messi la kukwepa kodi kutokana na mapato yatokanayo na jina na picha zake??
Sasa sakata hilo liko hivi.Maafisa wa kodi nchini Hispania wamemfutia makosa yote Lionel Messi hivyo hatakumbana na adhabu yoyote ile lakini baba mzazi wa mwanandinga huyo aitwaye Jorge Horacio Messi yuko hatarini kutupwa jela kwa kipindi cha miezi 18 na kulimwa faini ya paundi milioni 1.5 baada ya kukwepa kulipa kodi inayofikia paundi milioni 3 katika ya mwaka 2007-2009.
Taarifa zinadai kuwa Jorge Horacio Messi ndiye aliyehusika moja kwa moja na kosa hilo kwa kuwa yeye ndiye msimamizi wa mapato ya mwanaye na kwa kipindi kirefu amekuwa akikwepa kodi kwa kuficha mapato hayo kwenye mabenki ya Uruguay,Belize, Uswisi na Uingereza.
Mpaka sasa nyota watatu wa FC Barcelona,Lionel Messi,Neymar Jr na Javier Mascherrano wamejikuta wakiingia matatani kutoka na kulipa kodi zitokanazo na mapato ya haki za matumizi ya majina na picha zao.
0 comments:
Post a Comment