Nyota wa FC Barcelona Neymar Jr ndiye mwanasoka mwenye wafuasi wengi zaidi katika mtandao wa kijamii wa Instagram duniani kwa sasa akiwaacha nyuma magwiji wenzie Lionel Messi wa FC Barcelona na Cristiano Ronaldo wa Real Madrid.
Neymar Jr ana wafuasi milioni 32.6 idadi ambayo ina muweka juu ya Cristiano Ronaldo,mwenye wafuasi milioni 32,kisha Lionel Messi mwenye wafuasi milioni 25.7
Mpaka sasa mtandao wa Instagram una wafuasi wapatao milioni 400 duniani kote na kila siku picha zaidi ya milioni 80 huwekwa (upload) katika mtandao huo unaopendwa zaidi na vijana.
0 comments:
Post a Comment